Jana Machi 18, 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imelipongeza shirika lisililo la kiserikali linalotambulika kwa jina la PARTICIPATOR DEVELOPMENT CONCERN PADECO kwa kujenga Bweni moja na kukabidhi pikipiki mpya moja katika shule ya Elimu maalumu iliyopo Mundindi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Gilbert Ngailo ametoa pongezi hizo kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa shirika hilo mkoani Njombe na kusema serikali inashukuru kwa kujenga bweni lenye thamani ya shilingi 53,236,000 na pikipiki moja mpya yenye thamani ya shilingi 3,800,000.
Sambamba na hilo mwakilishi wa mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ametumia fursa hiyo kumwagiza Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw,AMOSI MTITU asimamie kikamilifu jengo hilo na pikipiki ambayo wamepewa kwaajili ya matumizi ya shule hiyo.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo Bi,Matha Mhagama amesema shirika hilo kwa kushirikiana na wafadhili kutoka ujerumani mwaka 2017 walifanikiwa kujenga bweni la wanafunzi wasichana katika shule hiyo na tayari linatumika.
Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Willbad Mwinuka amesema anaishuru Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa kuonesha ushirikiano wenye kuleta tija huku akiahidi kuendelea kufanya mambo mengi na yakimaendeleo katika halmashauri hiyo na kwingineko.
Tunashukuru
ReplyDeleteKaribu sana Ludewa iko salama
Delete