Mwenge wa Uhuru unaashiria nuru na mwanga.Uliwashwa kwa mara ya nchini
Tanzania juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro mwaka 1961.
Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 unatarajiwa kuwashwa rasmi Aprili 02,
2022 na Mwenge huo utawashwa katika Mkoa wa Njombe na baada ya hapo kuanza
rasmi kukimbizwa kwenye Wilaya za Mkoa wa Njombe na hatimaye kuukabidhi rasmi
katika Mkoa wa Ruvuma pale daraja la Ruhuhu lililopo Wilaya ya Ludewa.
Na kwa mwaka huu 2022 mwenge huu utakimbizwa mikoa yote nchini Tanzania na
kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa unatarajiwa kukimbizwa Aprili 07, 2022.
Mwenge huu unamulika nchini na nje ya mipaka ili kuleta matumaini pale
ambapo kuna kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale penye
dharau.
Sisi wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa tupo tayali kuupokea
mwenge wa uhuru kwenye Wilaya yetu na Kuilinda Amani na kudumisha Upendo.
Kila mwaka kuna mbio za mwenge zinazoanzia kwenye mikoa tofauti
kuwakumbusha Watanzania jukumu lao la kulinda uhuru, umoja na amani ambavyo
vimekuwepo na kudumu.
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa kutambua umuhimu na wajibu wetu wa
kulinda Uhuru Umoja na Amani ndani ya Halmashauri yetu tunasema karibu Mwenge
wa Uhuru Wilayani Ludewa,tupo tayali kuiangazia miradi ya kimaendeleo mikubwa
iliyo kamilika,inayo endelea na inayo tarajiwa kuanza.
Mwenge wa Uhuru kwa mawaka 2022 unakimbizwa ukiongozwa na kauli mbiu
isemayo,SENSA YA WATU NA MAKAZI:SENSA NI
MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO,SHIRIKI KUHESABIWA,TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA.
Sambamba na hayo mengi mazuri ya ujio wa mwengi kwenye Wilaya yetu ya
Ludewa,Tunaendelea na utoaji elimu kwa kila idara ambapo siku hiyo ya Mwenge
unapo wasili kwenye Wilaya yetu ya Ludewa tutatoa taarifa ya namna ambavyo
tunaendelea na utoaji elimu na Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI,MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA,MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA
KULEVYA,MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA,JINSI WILAYA INAVYO ELIMISHA WANANCHI KUHUSU
LISHE,MATUMIZI SAHIHI YA TEHAMA.
Kwa kauli hii ni dhaili Wilaya ya Ludewa tumejipanga vyema kuupokea
Mwenge wa uhuru na kuukaribisha uangaze kila pembe ya Wilaya ya Ludewa.
Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2022 ndani ya Halmashauri yetu utakesha
ukiangaza katika kata ya Manda kule kwenye kivutio kikubwa nchini Tanzania cha
Ziwa nyasa ukanda wa Ludewa.
Ni jukumu letu watanzania wote kuupokea mwenge wa uhuru na kuendelea
kudumisha Amani na Upendo tulio izoea kwenye nchi yetu nzuri ya Tanzania na
kutokomeza Ukatili,Ukabila,udini na rangi.
Ludewa ni Wilaya inayo funguka kwa uwekezaji na kwa nafasi hii nakuomba
wewe mtanzania mwenzangu karibu Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa,tunaviongozi
mahiri na shupavu na weredi katika majukumu yao,wakiongozwa na Mheshimiwa Mkuu
wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere na msimamizi na mtendaji mkuu wa Halmashauri
hiyo si mwingine bali ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa
Ndg.Sunday N. Deogratias
Mimi Chrispin Bernad Kalinga najivunia kuwapo Halmashauri ya
Wilaya ya Ludewa na ndio maana nimeona sasa nikupitishe kidogo ili uone shauku
ya kuja Ludewa,Miundombinu bora ya barabara,huduma za kijamii bila kusahau masuala
ya Afya kwenye Halmashauri yetu na nisipo gusia kwa uchache vivutio vya utalii
nitakuwa sijatenda haki.
Halmashauri yetu ya Wilaya ya Ludewa inafursa nyingi za uwekezaji
ikiwemo Kilimo,Ufugaji,Uvuvi na kubwa zaidi tunajivunia kuwa na Migodi mikubwa
ya Madini,Makaa ya Mawe,Chuma nk.
Halmashauri yetu inavivutio vingi vya utalii ambavyo sio rahisi
kuvimaliza vyote kwa ukrasa huu nitakuangazia vichache tu na,Kila kata ya
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa inautalii wake na kuvifanya vivutio vya Utalii
kuwa vingi na kuto tamani kuondoka Ludewa,tunajivunia kuwa na Mlima mkubwa wa
Livingstone,ambapo ndani yam lima huo kunavivutio vingi vya utalii yakiwemo
mapango,wanyama,ndege wadudu nk,na pia nikuangazie pale Ziwa nyasa ambapo tuna
tarafa ya Mwambao huko upo utalii ambao kwa siku 30 sio rahisi kuumaliza utalii
wengi tunafika na kujifunza vitu vingi mazingira yake hali ya hewa vinakufanya
usitamani kutoka katika Tarafa ya Mwambao.
Upo Utalii mwingi kwenye Halmashauri yetu Misitu ya asili Ngoma bora Duniani
ya Asili inayo julikana kwa jina la Mganda na nyingine Nyingi zinazo patikana
Ludewa pekee.
Sasa unashindwaje kufika Ludewa kuja kushuhudia mengi mazuri niliyo
kuangazia? Jibu la swahi hili unapaswa kulijibu kwa vitendo kwa kuchukua hatua
za haraka kuja Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kufanya uwekezai kuleta wageni
kutoka mataifa mbalimbali lakini watanzania wote Bara na Visiwani karibuni
Ludewa.
No comments:
Post a Comment