Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg.Sunday
Deogratias akiwa katika sherehe ya Wanawake Duniani,ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya
ya Ludewa ilifanyika siku ya jana Machi 08, 2022 katika Viwanja vya sokoni
Ludewa mjini aliongea na wakina mama walio jitokeza na kuwahidi kuwa serikali
ipo jirani na wakina mama.
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa
mwaka 2020/2021 imekopesha vikundi
mbalimbali vya wakina mama,vijana na watu wenye ulemavu,na kwa mwaka 2022/2023
bado inaendelea kukopesha fedha kwa vikundi vyote na akawataka wakina mama wote
wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa wafike katika ofisi za Maendeleo ya jamii kusajiliwa
vikundi na hatimaye wakopeshwe fedha.
,Natumia nafasi hii kuwakumbusha wakina mama wote wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ludewa kuwa, Halmashauri yetu inapesa isiyo na riba,jitokezeni mje
mkope na sisi kama Halmashuri tupo tayaali kuwapatieni,lakini pia nanyi vijana
wetu mliopo hapa pamoja na watu wenye ulemavu jitokezeni sajilini Vikundi njoeni
kopeni pesa,fedha hii ipo inawasubiri ninyi wenyewe’.
Hali kadhali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg.Sunday
Deogratius kupitia sherehe ya Wanawake Duniani,akawakumbusha wananchi wote wa Halmashauri
ya Wilaya ya Ludewa kutumia fursa ya utajiri mkubwa uliopa Wilayani Ludewa.
Wakina mama ludewa inafunguka,Fursa ya uwekezaji ni mkubwa,Wawekezaji
zaidi ya watatu tayali wamefika Ludewa na kuanza kuandaa mazingira ya kazi
kwenye migodi hapa Kwenye Wilaya yetu,anzeni kuweka mipango ya kuwahudumia
wageni kwa kuwauzia chakula,Jengeni nyumba za kulala wageni na kama huna pesa
kwani mgahawa unahitaji mtaji wa shilingi ngapi?fuata taratibu tukukopeshe
fedha ambayo haina riba,Wilaya hii inapokea wageni wengi watakosa kwa kulala
watakosa kwa kula kama msipo tumia fursa hii.
Lakini pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa
akaongeza kuwakaribisha watanzania wote walioko nje ya Ludewa na wageni wa
mataifa yote kuja kuwekeza Halmashauri ya Wilaya ya ludewa.

Ndugu zangu watanzania wote nawakaribisha Ludewa,Wilaya ya Ludewa ni
salama kwa uwekezaji ziko fursa nyingi za uwekezaji,karibuni kuwekeza
Ludewa,Kule Manda tuna ziwa nyasa ambalo ziwa hilo ni utalii tosha kwa Mkoa
wetu wa Njombe na Tanzania kwa ujumla wake,ukienda kule Lupingu,Makonde
utagundua mwambao inautalii wa kipekee hapa nchini Tanzania na duniani
kote,njoo wekezeni kwa ujenzi,biashara na mambo mengine maadamu tu hauvunji
sheria za nchi yetu,wazawa wa Wilaya ya Ludewa Mlioko nje ya Wilaya hii Leteni
wageni wawekeze nyumbani na ninyi wenyewe Ludini nyumbani kuwekeza na
kuibadilisha Ludewa,Ludewa sasa ni tajiri tunakila sababu ya kuja kufanya
uwekezaji.
No comments:
Post a Comment