Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Ludewa Ndg.Sunday Deogratius akiwakilishwa na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Gilbert Ngailo amekabidhiwa bweni moja la wanafunzi wa
wakiume katika Shule ya Msingi Mudindi ya watoto wenye mahitaji maalum iliyo
jengwa na Shirika la PADECO lenye thamani ya shilingi 53,236,000/=.
Aidha shirika
la PADECO licha ya kumkabidhi Kaimu Mkurugenzi bweni hilo likiwa limekamilika
wamemkabidhi bweni likiwa na vitanda pamoja na magodoro 50 na pikipiki mpya moja
yenye thamani ya shilingi 3,800,000/=
Kwa upande wake
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ludewa Ndg. Gilbert Ngailo amesema kuwa,
kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa amepokea
bweni hilo likiwa na vitanda na magodoro pamoja na pikipiki itakayo tumika
katika shule hiyo.
Sambamba na hayo Kaimu Mkurugenzi amempongeza Mkurugenzi wa Shirika la PADECO Ndg. Wilbard Mwinuka kwa uzalendo mkubwa anao ufanya kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa haswa katika miradi ya kimaendeleo.
Sambamba na hayo Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Wise Mgina ambaye pia ndiye Diwani Kata ya Mundindi amelipongeza Shirika la Padeco kwa mchango wao mkubwa haswa katika kufanikisha ujenzi wa bweni hili utakao saidia watoto wanao soma katika shule hiyo ya msingi ya watu wenye ulemavu.
Lakini pia akaongeza kwa kusema kuwa Shule hii ya watoto wenye ulemavu kwa Wilaya yetu ya Ludewa inapokea watoto kutoka maeneo tofauti nikiwa na maana ya ndani ya halmashauri ya Wilaya yetu na Mkoa mzima wa Njombe na pia saivi shule hii inapokea watoto kutoka nje ya Mkoa wa Njmbe,hivyo PADECO mchango wenu huu ni mkubwa tunawaomba msichoke kuja kuleta msaada na mahitaji mengine kadri mnavyo jaliwa.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa licha ya Shirika la Padeco kujenga bwini hili na serikali yetu pia imejenga jengo lingine kubwa ambalo lipo hatua za mwisho,hivyo nikiwa kama Mwenyekiti wa Halmashauri kwa umuhimu wa Shule hii,serikali inakila sababu ya kuona umuhimu wa kuongeza walimu katika shule hii ili waweze kutosheleza kuwahudumia watoto hawa,sambamba na hayo nitaenda kuishawishi serikali ione umuhimu wa kujenga na sekondari hapa,maana eneo bado lipo kubwa,na linauwezo wa kutosheleza kujenga shule ya sekondari ya watu wenye mahitaji maalumu,hii itasaidia mwenendo mzuri kwa wanafunzi wanao faulu kujinga na kidato cha kwanza,na sio hivyo tu bali nitaishawishi serikali kujenga chuo cha ufundi cha watu wenye mahitaji maalum ili waweze kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa upandewake mwenyekitiki wa chama cha mapinduzi CCM Ndg.Stanley Kolimba amesema kuwa,PADECO wanafanya mambo mengi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa haswa katika Miradi ya Maendeleo ya Afya,Elimu,Maji na mambo mbalimbali,sisi kama chama cha mapinduzi tunawapongeza Shirika la Padeco kwa kuona Umuhimu wa kuisaidia Wilaya ya Ludewa kwa Miradi mbalimbali na mambo haya mnayo yafanya PADECO ni mambo makubwa na yakuishi,hivyo nitumie nafasi hii kuwapongezeni.
Pia Mkurugenzi wa shirika la PADECO Ndg.Wilbard Mwinuka amesema kuwa,Sisi kama shirika lisilo la kiserikali,tumefanyanya mambo mengi kwenye Halmashauri ya Ludewa ikiwepo miradi ya ujenzi wa Vituo vya Afya,Ujenzi wa Vyumba vya Mdarasa na kusaidi a vikundi mbalimbali kwa kuviwezesha vifaa na mitaji ya kuanzia kazi.
Lakini kama shirika hatuchoki kuendelea kutenda matendo ya huruma sehemu mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
No comments:
Post a Comment