Ulaji mbaya wa chakula ni moja ya athari ambayo huathiri afya zetu na hapa ndipo watu wengi wana angukia, kuna makundi mawili ya ulaji mbaya wa chakula:-
1. Ratiba mbaya ya kula chalula.
Watu wengi hawana ratiba nzuri ya kula na wengi huchelewa kula kwa madai kazi zina watinga. Lakini ukweli ni kuwa ukichelewa kula una ua mwili wako taratibu, magonjwa kama vidonda vya tumbo yamekua yaki wasumbua watu wengi kutokana na kushindwa kula kwa wakati.
Kula usiku sana hupelekea mwili kutunza mafuta na ku ongezeka uzito. Kupoteza uwezo wa kufikiri,na kusinyaa kwa ubongo kutokana na kukosa cha nguvu kwa muda mrefu.
2. Kula vyakula hatarishi
Ulaji wa vyakula vya sukari kwa wingi,chumvi na kahawa hupelekea magonjwa kama shinikizo la damu na kusukari pia kuongezeka uzito kupunguza uwezo wa moyo kufanya kazi na kuathiri uwezo wa kufikiri.
Hivyo kwa nafasi hii ya kipekee nikukumbushe Mwananchi wa Wilaya ya Ludewa na Watanzania wote kwa Ujumla wake,ili kuepuka mathara yatokonayo na ulaji mbaya wa chakula, unachotakiwa kufuata ratiba ya kula, pia kuacha mara moja kula vyakula hatarishi.
No comments:
Post a Comment