Machi 09, 2022 Ofisi ya Kilimo na Umwagiliaji ya Wilaya ya Ludewa imeunda
jukwaa la uzalishaji wa Mbegu bora,akiongoza zoezi hilo wakati akitoa semina
kwa wadau,wakulima na wazalishaji wa mbegu mbalimbali,Tula Mlonge ambaye pia ni
kiongozi wa SACCOS SENTAR LIMITED amesema kuwa,lengo la kuja Halmashauri ya Wilaya
ya Ludewa ni kutokana na changamoto mbalimbali za mbegu bora kufika kwa
kuchelewa hupelekea wakulima kuto panda mbegu hizo kwa wakati.
Sambamba na mengine mengi Tula Mlenge amesema kuwa,Uwepo wa jukwaa hili Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa itamsaidia mkulima mdogo kuzifikia mbegu bora kwa urahisi na kwa haraka na akaongeza kwa kusema kuwa jukwaa hili litasaidia upatikanaji wa mbegu bora nyingi na kumrahisishia mkulima kuchagua mbegu anayo ihitaji.
Hali kadhalika ameongeza kwa kusema kuwa jukwaa hilo litakuwa ni jukwaa
la kutoa na kupokea taarifa kutoka kwa wakulima haswa wakati mkulima atakutana
na mbegu mbovu isiyo stawi ukilinganisha na wakati ulio pita ambapo mkulima
alikuwa haelewi wapi pa kwenda kuwasilisha lalamiko la kuuziwa mbugu isiyo
bora.
Kwa upande wake aliye chaguliwa leo na jukwaa la mbegu bora Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg.Teopista Mhagama kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo amesema,anaishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa uwepo wa wakulima kwenye Halmashauri ya Ludewa na ameahidi kuwa kwakushirikiana na viongozi wenza watahakikisha wanawaunganisha wakulima na serikali haswa kwenye changamoto ambazo wanakutana nazo na akaongeza kwa kusema kuwa kwa semina waliyo ipata leo wataendelea kutoa elimu kwa wakumima wote ili wakifikie kilimo biashara.
Pia wanachama wa jukwaa hilo kwa umoja wao wamekubaliana kuendelea kuwahimiza wakulima wengine kwa kwenda kutoa elimu ya umuhimu wa jukwaa hilo na kuongeza kusema kuwa jukwaa hilo limefika wakati muafaka kwenye Halmashauri ya Wilya ya Ludewa.
No comments:
Post a Comment