March 23, 2022

FURSA ZA KILIMO CHA KAHAWA LUDEWA

Wakati ukijiuliza wapi zinapatika fursa za kilimo hapa nchini Tanzania leo nakunong'oneza kwa ukaribu kuwa Halmashari ya Wilaya ya Ludewa inamaeneo ya mengi ya  wazi kwaajili ya kilimo.

Na ikumbukwe kwamba Udongo wa Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa hauchagui zao lipi la falaa kwa kilimo jibu ni kwamba mazao yote yanastahili ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.

Hivi karibuni Meneja wa Kanda za juu Kusini Bw.Ferouz Mkongo alitembea baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na kushuhudia haya ninayo kueleza.

Bw.Ferouz Mkongo alisema lengo kubwa la kutembelea maeneo hayo ni pamoja na kuwasaidia wakulima wa zao la Kahawa,Korosho,Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa na samaki kupatiwa mikopo ya asilimia 9 kwa mwaka kwenye minyololo ya thamani ya mazao tajwa hapo juu.

Katika kufanikisha hayo Bw. Ferouz aliambatana na Kaimu Afisa Kilimo  Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Ludewa Clementina Kabaka na moja ya wakulima walio fikiwa ni pamoja na Mkulima wa Kijiji cha Lufumbu ambaye pia ni mkulima bora wa zao la Kahawa 

March 22, 2022

TAARIFA KWA UUMA



Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa POLIO nchini Malawi, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa itaanza zoezi la kampeni ya utoaji wa chanjo ya matone ya kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (5).

 Chanjo itaanza kutolewa kuanzia tarehe 27 Machi 2022, saa 1:30 asubuhi katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya, pia timu ya watalamu na wahamasishaji watapita nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuhamasisha watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano (5) wapate chanjo.

 Aidha katika kampeni hii watoto wote ambao walichanja na wale ambao hawakuchanja chanjo ya matone ya POLIO watapatiwa chanjo ili kuwakinga na mlipuko wa POLIO ulio tangazwa nchini Malawi.

 Chanjo ya matone ya POLIO inasaidia kuimarisha kinga ya mtoto dhidi ya maambukizi na madhara ya ugonjwa wa POLIO ambao ni ulemavu wa viungo na vifo kwa watoto.

 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere, anatoa wito kwa wazazi/walezi wenye watoto chini ya umri wa miaka mitano (5) wahakikishe wanawafikisha watoto hao kwenye vituo vya afya ili wapatiwe chanjo ya POLIO.

March 21, 2022

KAIMU MKURUGENZI WILAYA YA LUDEWA AAGIZA ELIMU YA KULIFIKIA DAWATI LA JINSIA IWAFIKIE WANANCHI ITAPUNGUZA UKATILI DHIDI YA WATOTO NA WANAWAKE



Leo Machi 21, 2022 Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Ludewa Bw. Gilbert Ngailo ameongoza kikao cha robo tatu ya kamati ya Wilaya ya Kupinga ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake.

Aidha wakati wa kikao hicho PC. Mwanaisha S. Hamisi wa Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi Wilaya ya Ludewa,pamoja na mambo mengine amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Afua za kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na wanawake kwa kipindi cha kuanzia Mwenzi Januari hadi Machi 2022.

Akaongeza kwa kusema kuwa Dawati la Jinsia la Polisi lipo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa hivyo anawaomba wananchi kutoa taarifa za Ukatili kwenye Dawati hilo popote ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwenye Vituo vya Polisi.

Kwa upande wake Mjumbe wa kikao hicho Sheikh wa Wilaya ya Ludewa Haruna Rahim amemuomba Kaimu Mwenyekiti wa kikao cha robo tatu ya kamati ya Wilaya ya Kupinga Ukatili dhidi ya Watoto na Mwanamke Ndg.Gilbert Ngailo,kuwa anaomba lianzishwe na Jukwaa la ukatili dhidi ya wanaume wanao fanyiwa ukatili lianzishwe.

Aidha wakati wa majadiliano hayo juu ya ombi la Sheikh Haruna Rahim kuomba kuanzishwe Jukwaa la Ukatili dhidi ya wanaume wanao fanyiwa ukatili lianzishwe, Mjumbe wa Kikao hicho Afisa Mradi wa Mwanamke imara kutoka Shirika la WILDAF Mkoa wa Njombe amejibu ombi la Sheikh Haruna Rahim kuwa Dawati la Jinsia na Watoto ,lipo kwa lengo la kusikiliza na kuchukua hatua stahiki kwa wale walio fanyiwa ukatili,lakini uwepo wa Dawati hilo haimaanishi kwamba wanao takiwa kwenda kupeleka ukatili huo ni watoto na wakinamama tu,Hapana bali Dawati hilo lipo kwaajili ya wote,Ukatili dhidi ya watoto,Wanawake na Wanaume.

Sambamba na hayo Mwenyekiti wa kikao hicho Ndg. Gilbert Ngailo amewasisitiza wajumbe wote kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waondokane na Ukatili kwa watu wote.

Sambamba na hayo akaongeza kwa kusema kuwa tunapo zungumzia ukatili tunazungumzia Ukatili wa Kimwili,Ukatili wa Kiuchumi,Ukatili wa Kihisia na Ukatili wa Kingono.

March 19, 2022

LUDEWA NI WILAYA ILIYO BARIKIWA NCHINI TANZANIA



Ninapo zungumzia Fursa za Uwekezaji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ninamaanisha zipo fursa nyingi kama ifuatavyo:-

Tuko na Fursa za Kilimo
Fura ya Mifugo
Fursa za Utalii
Fursa za Madini

Wilaya yetu ya Ludewa imejaliwa kuzungukwa na ukijani mbichi kila mahali na Milima mizuri inayo vutia kuitizama na kuona kama uko Dunia ya zaidi ya Dunia.

Hapa nakuangazia tu Moja ya Vivutio vinavyo tamanisha wengi kuja kutalii na mimi pia nakukaribisha sana kuja kufanya Utalii wewe mwenyewe.

Tuko na Utalii wa Ziwanyasa,Mungu hakuacha kutupatia Ziwanyasa ukanda wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ambako sasa ni Tarafa ya mwambo,huko kuna utalii ndani ya Ziwanyasa,utakutana na maji ya aina yake ndani ya ziwanyasa,Mchanga unao patikana ziwanyasa ukanda wa Ludewa ni tofauti kabisa,Utagundua Mikondo ya maji ya ziwanyasa ni tofauti na mikondo mingine iliyo zoeleka,na kwa upande wa mawe mapambo ya ziwanyasa ndio usiseme kabisa,ukiwa kama unaelekea Mbeya kule kunako itwa Makonde hauto juta kufika kutizama milima iliyo jipanga kwa ngazi moja na nyingine.

hapo nimekusogezea vichache tu ukiondoa samaki wenye rangi alimaarufu kwa samaki wa mapambo,je Utafikaje kote huko ? jibu ni kwamba Karibu Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri utapata maelekezo yaliyo jitosheleza nami nitaambatana nawe hadi kote ukutakako

Ludewa ni Wilaya iliyo barikiwa nchini Tanzania

HALMASHAURI LUDEWA YATOA VYANDUA 80 KATIKA SHULE YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM MUNDINDI



Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imetoa Vyandarua 80 katika shule ya msingi Mundindi ya watu wenye mahitaji maalum

Akikabidhi vyandurua hivyo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Gilbert Ngailo ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg Sunday Deogratias kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya shirika la PADECO.

Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Leo Machi 18, 2022 nimekuja kupokea bweni moja na pikipiki mliyo tuwezesha ninyi shirika la Padeco,tunawashukuru sana na Mkurugenzi amesema nizilete kwenu shukrani hizi,nasi kama halmashauri kwa kutambua uwepo wa watoto hawa nasi tunatoa Vyandarua hivi 80 ili kuendelea kupambana na Maralia.alisema Gilbert Ngailo.

MWENYEKITI WA CCM LUDEWA ATOA TAMKO



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ludewa Ndg. Stanley Kolimba Jana Machi 18, 2022 alizungumza na wananchi walio jitokeza katika hafla ya Miaka 10 ya shirika la PADECO walio jitokeza katika Kata ya Mundindi  shule ya msingi ya watu wenye mahitaji maalum.

Ndg.Stanlye Kolimba alisema kuwa katika kipindi cha Mwaka mmoja wa uongozi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa amefanya mambo mengi ikiwemo Miradi ya Maendeleo ya Afya,Miradi ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa na Miundombinu ya Barabara.
 
Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo aliongeza kwa kusema kuwa, tunakila sababu ya kumshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maendeleo anayo yaleta nchi kwetu haswa kwenye miradi inayo ishi, ikumbukwe kwamba Mwaka huu 2022 Mhe.Rais ametupati Fedha nyingi ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA pale Shaurimoyo ambapo ujenzi wake tayali umeanza na utarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Katika hatua nyingine Kolimba alisema Shirika la Padeco ni moja ya mashirika yanayo hitaji kuigwa haswa kwa kurudisha fadhira ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na akatumia nafasi hiyo Kumpongeza Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Wilbaard Mwinuka kwa kuendelea kuijenga Wilaya ya Ludewa kwa miradi ya kimaendeleo.

Nakupongeza kijana wetu kwa kuona umuhimu wa kuja kusaidia wototo hawa na kuwapa zawadi Bweni hili pamoja na vitanda,Magodoro 50 bado ukajenga na vyoo vitano na ukaongeza Usafiri wa pikipiki wa kuwahudimia pindi wanapo pata shida Hongera sana kijana,Sisi kama chama cha mapinduzi Wilaya ya Ludewa tunautambua Mchango wako kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa,endelea hivyo hivyo na moyo wa upendo.

Wilaya yetu inafunguka kwa mambo mengi endelea kukaribisha wageni kutoka maeneo yote waje wawekeze kwenye Halmashauri yetu uchumi Utaongezeka.


Kwa upande wake Kaimu Katibu wa wazazi CCM Wilaya ya Ludewa Ndg. Salum Mohamed Mfaume alisema kuwa uwepo wa bweni hilo ambalo Shirika la PADECO limeiwezesha shule hiyo itawafanya watoto wanao soma hapo kuishi vizuri na furaha wakiyafurahia mazingira hayo, aliendelea kusema kusema kuwa watoto ni Taifa la kesho hivyo kila mtoto aliye zaliwa anahaki ya kupata elimu kwa kauli mbiu isemayo, Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.


Bw. LINUS MALAMBA ASIMAMIA SEMINA YA UGONJWA WA POLIO


Leo Machi 19, 2022 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ludewa atoa semina ya Mafunzo kwa Kamati ya Msingi ya Afya ngazi ya Jamii (PHC) na Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ludewa akiliwakilishwa na Kaimu Das Wilaya ya Ludewa Bw. Linus Malamba



Pamoja na mambo mengine Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bw.Stanley Mlay amewaelekeza wajumbe wote walio hudhulia kikao chicho kuwa wakawe mstari wa mbele Kuongeza uelewa kwa wanajamii kuhusu faida za chanjo ya Polio.

#endelea kutembelea mitandao yetu ya kijamii kwa habari zote.

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA PADECO AISHUKURU HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA




Jana Machi 18, 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa  imelipongeza shirika lisililo la kiserikali linalotambulika kwa jina la PARTICIPATOR DEVELOPMENT CONCERN PADECO kwa kujenga Bweni moja na kukabidhi pikipiki mpya moja katika shule ya Elimu maalumu iliyopo Mundindi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa  Ndg. Gilbert Ngailo ametoa pongezi hizo kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa shirika hilo mkoani Njombe na kusema serikali inashukuru kwa kujenga bweni lenye thamani ya shilingi 53,236,000 na pikipiki moja mpya yenye thamani ya shilingi 3,800,000.



Sambamba na hilo mwakilishi wa mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ametumia fursa hiyo kumwagiza Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw,AMOSI MTITU asimamie kikamilifu jengo hilo na pikipiki ambayo wamepewa kwaajili ya matumizi ya shule hiyo.


Awali akisoma taarifa ya mradi huo Bi,Matha Mhagama amesema shirika hilo kwa kushirikiana na wafadhili kutoka ujerumani mwaka 2017 walifanikiwa kujenga bweni la wanafunzi wasichana katika shule hiyo na tayari linatumika.



Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Willbad Mwinuka amesema anaishuru Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa kuonesha ushirikiano wenye kuleta tija huku akiahidi kuendelea kufanya mambo mengi na yakimaendeleo katika halmashauri hiyo na kwingineko.




March 18, 2022

MHE.WISE MGINA ATOA NENO LA NEEMA SHULE YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM







Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ludewa Ndg.Sunday Deogratius akiwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Gilbert Ngailo amekabidhiwa bweni moja la wanafunzi wa wakiume katika Shule ya Msingi Mudindi ya watoto wenye mahitaji maalum iliyo jengwa na Shirika la PADECO lenye thamani ya shilingi 53,236,000/=.



Aidha shirika la PADECO licha ya kumkabidhi Kaimu Mkurugenzi bweni hilo likiwa limekamilika wamemkabidhi bweni likiwa na vitanda pamoja na magodoro 50 na pikipiki mpya moja yenye thamani ya shilingi 3,800,000/=








Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ludewa Ndg. Gilbert Ngailo amesema kuwa, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa amepokea bweni hilo likiwa na vitanda na magodoro pamoja na pikipiki itakayo tumika katika shule hiyo.






Sambamba na hayo Kaimu Mkurugenzi amempongeza Mkurugenzi wa Shirika la PADECO Ndg. Wilbard Mwinuka kwa uzalendo mkubwa anao ufanya kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa haswa katika miradi ya kimaendeleo.



Sambamba na hayo Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Wise Mgina ambaye pia ndiye Diwani Kata ya Mundindi amelipongeza Shirika la Padeco kwa mchango wao mkubwa haswa katika kufanikisha ujenzi wa bweni hili utakao saidia watoto wanao soma katika shule hiyo ya msingi ya watu wenye ulemavu.



Lakini pia akaongeza kwa kusema kuwa Shule hii ya watoto wenye ulemavu kwa Wilaya yetu ya Ludewa inapokea watoto kutoka maeneo tofauti nikiwa na maana ya ndani ya halmashauri ya Wilaya yetu na Mkoa mzima wa Njombe na pia saivi shule hii inapokea watoto kutoka nje ya Mkoa wa Njmbe,hivyo PADECO mchango wenu huu ni mkubwa tunawaomba msichoke kuja kuleta msaada na mahitaji mengine kadri mnavyo jaliwa.



Aidha ameongeza kwa kusema kuwa licha ya Shirika la Padeco kujenga bwini hili na serikali yetu pia imejenga jengo lingine kubwa ambalo lipo hatua za mwisho,hivyo nikiwa kama Mwenyekiti wa Halmashauri kwa umuhimu wa Shule hii,serikali inakila sababu ya kuona umuhimu wa kuongeza walimu katika shule hii ili waweze kutosheleza kuwahudumia watoto hawa,sambamba na hayo nitaenda kuishawishi serikali ione umuhimu wa kujenga na sekondari hapa,maana eneo bado lipo kubwa,na linauwezo wa kutosheleza kujenga shule ya sekondari ya watu wenye mahitaji maalumu,hii itasaidia mwenendo mzuri kwa wanafunzi wanao faulu kujinga na kidato cha kwanza,na sio hivyo tu bali nitaishawishi serikali kujenga chuo cha ufundi cha watu wenye mahitaji maalum ili waweze kujifunza mambo mbalimbali.





Kwa upandewake mwenyekitiki wa chama cha mapinduzi CCM Ndg.Stanley Kolimba amesema kuwa,PADECO wanafanya mambo mengi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa haswa katika Miradi ya Maendeleo ya Afya,Elimu,Maji na mambo mbalimbali,sisi kama chama cha mapinduzi tunawapongeza Shirika la Padeco kwa kuona Umuhimu wa kuisaidia Wilaya ya Ludewa kwa Miradi mbalimbali na mambo haya mnayo yafanya PADECO ni mambo makubwa na yakuishi,hivyo nitumie nafasi hii kuwapongezeni.



Pia Mkurugenzi wa shirika la PADECO Ndg.Wilbard Mwinuka amesema kuwa,Sisi kama shirika lisilo la kiserikali,tumefanyanya mambo mengi kwenye Halmashauri ya Ludewa ikiwepo miradi ya ujenzi wa Vituo vya Afya,Ujenzi wa Vyumba vya Mdarasa na kusaidi a vikundi mbalimbali kwa kuviwezesha vifaa na mitaji ya kuanzia kazi.



Lakini kama shirika hatuchoki kuendelea kutenda matendo ya huruma sehemu mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na  nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.


March 17, 2022

LUDEWA TWAMKUMBUKA Dkt.JOHN POMBE MAGUFULI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Watanzania katika Maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwaka Mmoja wa kifo cha Hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais ya Awamu ya Tano.

Nasi Wananchi wa Wilaya ya Ludewa tumejumuika na Mhe. Rais katika kumbukizi hii kwa kuyakumbuka mambo mengi aliyo yafanya enzi za uhai wake Hayati Dkt.John Pombe Maguli.

JE , WAJUA KUWA KUTO FUATA RATIBA YA KULA HUATHIRI AFYA YA MWILI?



Kuna tabia ambazo zimekuwa zikiathiri afya zetu kwa kiwango kikubwa. Kuna wakati tunafanya hivyo aidha kwa kutokujua au kwa kujua. Hivyo miongoni mwa tabia hizo ambazo huathiri afya zetu kwa kiwango kikubwa ni kama ifuatavyo;

Ulaji mbaya  wa chakula ni moja ya athari ambayo huathiri afya zetu na hapa ndipo watu wengi wana angukia, kuna makundi mawili ya ulaji mbaya wa chakula:-

1. Ratiba mbaya ya kula chalula.

Watu wengi hawana ratiba nzuri ya kula na wengi huchelewa kula kwa madai kazi zina watinga. Lakini ukweli ni kuwa ukichelewa kula una ua mwili wako taratibu, magonjwa kama vidonda vya tumbo yamekua yaki wasumbua watu wengi kutokana na kushindwa kula kwa wakati.

Kula usiku sana hupelekea mwili kutunza mafuta na ku ongezeka uzito. Kupoteza uwezo wa kufikiri,na kusinyaa kwa ubongo kutokana na kukosa cha nguvu kwa muda mrefu.

2. Kula vyakula hatarishi

Ulaji wa vyakula vya sukari kwa wingi,chumvi na kahawa hupelekea magonjwa kama shinikizo la damu na kusukari pia kuongezeka uzito kupunguza uwezo wa moyo kufanya kazi na kuathiri uwezo wa kufikiri.

Hivyo kwa nafasi hii ya kipekee nikukumbushe Mwananchi wa Wilaya ya Ludewa na Watanzania wote kwa Ujumla wake,ili kuepuka mathara yatokonayo na ulaji mbaya wa chakula, unachotakiwa kufuata ratiba ya kula, pia kuacha mara moja kula vyakula hatarishi.

MAANDALIZI YA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU WILAYA YA LUDEWA YANAENDELEA



Kikao cha nne cha sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru kinaendelea leo Machi 17, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na Mwenyekiti wa kikao hicho akiwa ni Kaimu DAS  Bw.Linus Malamba akimuwakilisha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere na katibu wa kikao hicho akiwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Gilbart Ngailo akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias.















Moja ya mambo yanayo jadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na Mapitio ya bajeti za kamati mbalimbali za sherehe za Mbio za Mwenge wa uhuru 2020.








Aidha wajumbe mbalimbali wamehudhulia kikao hicho ikiwemo kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ludewa,Viongozi wa madhehebu ya dini,Viongozi wa Chama cha cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti wa wafanya biashara,Wazee maarufu pamoja na wadau wengine.




Ikumbukwe kwamba Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2022 unatarajiwa kuwashwa rasmi tarehe 02 Aprili 2022 katika Mkoa wa Njombe ndani ya Uwanja wa Sabasaba Njombe na kwa Wilaya ya Ludewa tunatarajia kuupokea Mwenge huo Tarehe 07 Aprili 2022




Aidha  Mwenge wa Uhuru kwa siku hiyo ya Aprili 7, 2022 utakesha Manda na Tarehe 08 Aprili 2022  utakabidhiwa Mkoa wa Ruvuma daraja la mto Ruhuhu.





March 16, 2022

WANANCHI LUDEWA TWAUNGANA NA Mhe. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN





Siku kama ya leo Machi 17, 2021 ilikuwa ya majonzi kwa Watanzania, baada ya Rais wa awamu ya 5 Hayati Dkt. John Magufuli kufariki dunia.

Rais Samia Suluhu Hassan Leo Machi 17,2022 ataongoza Watanzania katika kumbukizi hii ya mwaka mmoja ya kifo cha Magufuli itakayofanyika katika Uwanja wa Magufuli Chato Mkoani Geita.

Nasi wananchi wa Wilaya ya Ludewa Leo tunaungana na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha Dkt. John Pombe Magufuli (1959-2021), Rais wa awamu ya tano wa Tanzania.
Dkt. Magufuli aliyeiongoza Tanzania kwa miaka mitano na miezi minne alifariki Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam kutokana na tatizo la moyo.

Daima Wanaludewa na Watanzania wote tutakukumbuka Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Endelea kupumzika kwa amani.

MWENYEKITI WA HALMASHAURI (W) LUDEWA,ANENA NENO




Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Ludewa Wise Mgina Jana Machi 15, 2022 alitembelea Msitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ulioko Kata ya Madope ambao uliungua na moto mwishoni mwa mwaka 2021.

Katika hatua nyingine Mhe. Mwenyekiti Wise Mgina alipo kuwa akikagua msitu huo alisema kuwa,"Msitu huu ni msitu ambao ulikuwa ni sehemu ya utajiri wa Halmashauri yetu,lakini moto ulivamia na kutuingiza hasara ya kuanza kuvuna miti hii kwa muda usio pangwa.


Mhe.Mgina aliongeza kwa kusema kuwa,Licha ya hasara ambayo imejitokeza hatuwezi acha miti hii ikauke,sisi kama Halmashauri tumeamua tuuchane mbao wenyewe.

Ikumbukwe kwamba Mwezi Januari 10 Mwaka huu Halmashauri ilitangaza kuuzwa kwa miti hiyo ambapo walijitokeza wanunuzi mbalimbali na kutaka kuununua kwa bei chini na uongozi wahalmashauri haikusita kusitisha kuuza msitu huo kwa hasara.


Hali kadhalika Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Wise Mgina aliongeza kwa kusema kuwa,Wengi wamekuja wakitaka kununua miti hii iliyo ungua kwa bei ndogo lakini sisi kama Halmashauri tumekataa tumeamua kuuchana wenyewe,kwa hatua hii tulio ichukua tunatarajia kupa mbao zaidi ya 50,000 zinapatika hapa,na mbao hizi zikipatikana zitatumika kwenye majengo ya Serikali yanayo jengwa sasa na yatakayo jengwa baadae.

Pia alimaliza kwa kusema kuwa' wananchi wote wa Wilaya ya Ludewa natumia nafasi hii kuwasihi acheni kuchoma moto ovyo, mnairudisha halmashauri yetu nyuma kwa kuharibu miti,ipo miti mingi ndani ya Halmashauri hii imeungua na haijafikia kiwango cha kupasuliwa tufuate taratibu za kupata kibali cha kuchoma moto kutoka kwenye serikali ya vijiji vyetu.


LUDEWA YAPIGA HATUA ANWANI ZA MAKAZI



Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias anawajuza wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuwa, katika zoezi la Utoaji elimu ya mfumo wa anwani za makazi kwa Watumishi wote wa Tarafa 5 watakao waongoza vijana walio chaguliwa kutoka kwenye kata zote za Wilaya ya Ludewa limekamilika Jana Machi15, 2022.

Aidha anapenda kuwajuza kuwa, zoezi linalo fuata sasa ni kuwapa semina elekezi ya namna ya kuchukua taarifa kwa usahihi na kuzitunza katika mfumo.

Vijana wote wenye sifa walio chaguliwa kutoka kwa watendaji wa Kata, hivi karibuni mtapewa taarifa ya lini na muda gani mtapaswa kuja kupewa semina.

Lakini pia Ndg Sunday Deogratias anawaomba wanachi wote pindi vijana hao watakapo anza kupita kwenye makazi yao kwaajili ya kuchukua taarifa muwape ushirikiano ili kukamilisha zoezi hili kwa muda ulio pangwa.


Usisahau kutembelea kurasa zetu za mitandao ya kijamii {Twitter "Halmashauri Ludewa" Blog "Halmashauriludewa.blogspot.com" na YOU TUBE CHANEL kwa jina la "Halmashauri Ludewa".

March 10, 2022

NEEMA YA MAJI YAMWAGIKA MADINDO

Diwani wa Kata ya Ludende Mhe.Vasco Mgimba ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha kuwapelekea maji wananchi wa Kijiji cha Madindo Kata ya Ludende Wilaya ya Ludewa.

 Akizungumza hayo Jana Machi 09, 2022 wakati akikagua miundombinu ya maji inayo jengwa na RUWASA,”Tunakila sababu ya kumshuuru Mheshimiwa Rais Kwa kuona wananchi wanavyo teseka na upatikanaji wa maji,leo maji yanatoka hivi ujue Rais kasikia kilio chetu’. Amesema  Vasco Mgimba  



 Sambamba na hayo akaongeza kwa kusema kuwa wananchi wa Kata ya Ludende sasa maji safi na salama yamepatikana wanapaswa kuilinda na kuitunza miundombinu hiyo ili isaidie kizazi cha leo na cha baadaye.



 Wananchi wa kijiji cha Mandindo Kata ya Ludende Baada ya kusubiri kwa muda mrefu kupata maji sasa mnakila sababu ya kuilinda miundombinu hii ili isaharibiwe na yeyote,Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imekelezwa hapa leo kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ya chama change, moja ya vipaumbele vyake ni kuhakikisha wananchi wanaondokana kwenye changamoto ya upatikanaji wa maji. Amesema  Vasco Mgimba

March 09, 2022

LUDEWA YAJIPANGA KUPOKEA MWENGE WA UHURU KWA KISHINDO 2022




Mwenge wa Uhuru unaashiria nuru na mwanga.Uliwashwa kwa mara ya nchini Tanzania juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro mwaka 1961.

Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 unatarajiwa kuwashwa rasmi Aprili 02, 2022 na Mwenge huo utawashwa katika Mkoa wa Njombe na baada ya hapo kuanza rasmi kukimbizwa kwenye Wilaya za Mkoa wa Njombe na hatimaye kuukabidhi rasmi katika Mkoa wa Ruvuma pale daraja la Ruhuhu lililopo Wilaya ya Ludewa.

Na kwa mwaka huu 2022 mwenge huu utakimbizwa mikoa yote nchini Tanzania na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa unatarajiwa kukimbizwa Aprili 07, 2022.

Mwenge huu unamulika nchini na nje ya mipaka ili kuleta matumaini pale ambapo kuna kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale penye dharau.




Sisi wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa tupo tayali kuupokea mwenge wa uhuru kwenye Wilaya yetu na Kuilinda Amani na kudumisha Upendo.

Kila mwaka kuna mbio za mwenge zinazoanzia kwenye mikoa tofauti kuwakumbusha Watanzania jukumu lao la kulinda uhuru, umoja na amani ambavyo vimekuwepo na kudumu.

Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa kutambua umuhimu na wajibu wetu wa kulinda Uhuru Umoja na Amani ndani ya Halmashauri yetu tunasema karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Ludewa,tupo tayali kuiangazia miradi ya kimaendeleo mikubwa iliyo kamilika,inayo endelea na inayo tarajiwa kuanza.

Mwenge wa Uhuru kwa mawaka 2022 unakimbizwa ukiongozwa na kauli mbiu isemayo,SENSA YA WATU NA MAKAZI:SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO,SHIRIKI KUHESABIWA,TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA.

Sambamba na hayo mengi mazuri ya ujio wa mwengi kwenye Wilaya yetu ya Ludewa,Tunaendelea na utoaji elimu kwa kila idara ambapo siku hiyo ya Mwenge unapo wasili kwenye Wilaya yetu ya Ludewa tutatoa taarifa ya namna ambavyo tunaendelea na utoaji elimu na Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI,MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA,MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA,MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA,JINSI WILAYA INAVYO ELIMISHA WANANCHI KUHUSU LISHE,MATUMIZI SAHIHI YA TEHAMA.



Kwa kauli hii ni dhaili Wilaya ya Ludewa tumejipanga vyema kuupokea Mwenge wa uhuru na kuukaribisha uangaze kila pembe ya Wilaya ya Ludewa.

Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2022 ndani ya Halmashauri yetu utakesha ukiangaza katika kata ya Manda kule kwenye kivutio kikubwa nchini Tanzania cha Ziwa nyasa ukanda wa Ludewa.

Ni jukumu letu watanzania wote kuupokea mwenge wa uhuru na kuendelea kudumisha Amani na Upendo tulio izoea kwenye nchi yetu nzuri ya Tanzania na kutokomeza Ukatili,Ukabila,udini na rangi.

Ludewa ni Wilaya inayo funguka kwa uwekezaji na kwa nafasi hii nakuomba wewe mtanzania mwenzangu karibu Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa,tunaviongozi mahiri na shupavu na weredi katika majukumu yao,wakiongozwa na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere na msimamizi na mtendaji mkuu wa Halmashauri hiyo si mwingine bali ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg.Sunday N. Deogratias

Mimi Chrispin Bernad Kalinga najivunia kuwapo Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na ndio maana nimeona sasa nikupitishe kidogo ili uone shauku ya kuja Ludewa,Miundombinu bora ya barabara,huduma za kijamii bila kusahau masuala ya Afya kwenye Halmashauri yetu na nisipo gusia kwa uchache vivutio vya utalii nitakuwa sijatenda haki.

Halmashauri yetu ya Wilaya ya Ludewa inafursa nyingi za uwekezaji ikiwemo Kilimo,Ufugaji,Uvuvi na kubwa zaidi tunajivunia kuwa na Migodi mikubwa ya Madini,Makaa ya Mawe,Chuma nk.

Halmashauri yetu inavivutio vingi vya utalii ambavyo sio rahisi kuvimaliza vyote kwa ukrasa huu nitakuangazia vichache tu na,Kila kata ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa inautalii wake na kuvifanya vivutio vya Utalii kuwa vingi na kuto tamani kuondoka Ludewa,tunajivunia kuwa na Mlima mkubwa wa Livingstone,ambapo ndani yam lima huo kunavivutio vingi vya utalii yakiwemo mapango,wanyama,ndege wadudu nk,na pia nikuangazie pale Ziwa nyasa ambapo tuna tarafa ya Mwambao huko upo utalii ambao kwa siku 30 sio rahisi kuumaliza utalii wengi tunafika na kujifunza vitu vingi mazingira yake hali ya hewa vinakufanya usitamani kutoka katika Tarafa ya Mwambao.

Upo Utalii mwingi kwenye Halmashauri yetu Misitu ya asili Ngoma bora Duniani ya Asili inayo julikana kwa jina la Mganda na nyingine Nyingi zinazo patikana Ludewa pekee.

Sasa unashindwaje kufika Ludewa kuja kushuhudia mengi mazuri niliyo kuangazia? Jibu la swahi hili unapaswa kulijibu kwa vitendo kwa kuchukua hatua za haraka kuja Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kufanya uwekezai kuleta wageni kutoka mataifa mbalimbali lakini watanzania wote Bara na Visiwani karibuni Ludewa.

FURSA ZA KILIMO CHA KAHAWA LUDEWA

Wakati ukijiuliza wapi zinapatika fursa za kilimo hapa nchini Tanzania leo nakunong'oneza kwa ukaribu kuwa Halmashari ya Wilaya ya Ludew...