March 23, 2022

FURSA ZA KILIMO CHA KAHAWA LUDEWA

Wakati ukijiuliza wapi zinapatika fursa za kilimo hapa nchini Tanzania leo nakunong'oneza kwa ukaribu kuwa Halmashari ya Wilaya ya Ludewa inamaeneo ya mengi ya  wazi kwaajili ya kilimo.

Na ikumbukwe kwamba Udongo wa Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa hauchagui zao lipi la falaa kwa kilimo jibu ni kwamba mazao yote yanastahili ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.

Hivi karibuni Meneja wa Kanda za juu Kusini Bw.Ferouz Mkongo alitembea baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na kushuhudia haya ninayo kueleza.

Bw.Ferouz Mkongo alisema lengo kubwa la kutembelea maeneo hayo ni pamoja na kuwasaidia wakulima wa zao la Kahawa,Korosho,Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa na samaki kupatiwa mikopo ya asilimia 9 kwa mwaka kwenye minyololo ya thamani ya mazao tajwa hapo juu.

Katika kufanikisha hayo Bw. Ferouz aliambatana na Kaimu Afisa Kilimo  Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Ludewa Clementina Kabaka na moja ya wakulima walio fikiwa ni pamoja na Mkulima wa Kijiji cha Lufumbu ambaye pia ni mkulima bora wa zao la Kahawa 

March 22, 2022

TAARIFA KWA UUMA



Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa POLIO nchini Malawi, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa itaanza zoezi la kampeni ya utoaji wa chanjo ya matone ya kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (5).

 Chanjo itaanza kutolewa kuanzia tarehe 27 Machi 2022, saa 1:30 asubuhi katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya, pia timu ya watalamu na wahamasishaji watapita nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuhamasisha watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano (5) wapate chanjo.

 Aidha katika kampeni hii watoto wote ambao walichanja na wale ambao hawakuchanja chanjo ya matone ya POLIO watapatiwa chanjo ili kuwakinga na mlipuko wa POLIO ulio tangazwa nchini Malawi.

 Chanjo ya matone ya POLIO inasaidia kuimarisha kinga ya mtoto dhidi ya maambukizi na madhara ya ugonjwa wa POLIO ambao ni ulemavu wa viungo na vifo kwa watoto.

 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere, anatoa wito kwa wazazi/walezi wenye watoto chini ya umri wa miaka mitano (5) wahakikishe wanawafikisha watoto hao kwenye vituo vya afya ili wapatiwe chanjo ya POLIO.

March 21, 2022

KAIMU MKURUGENZI WILAYA YA LUDEWA AAGIZA ELIMU YA KULIFIKIA DAWATI LA JINSIA IWAFIKIE WANANCHI ITAPUNGUZA UKATILI DHIDI YA WATOTO NA WANAWAKE



Leo Machi 21, 2022 Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Ludewa Bw. Gilbert Ngailo ameongoza kikao cha robo tatu ya kamati ya Wilaya ya Kupinga ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake.

Aidha wakati wa kikao hicho PC. Mwanaisha S. Hamisi wa Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi Wilaya ya Ludewa,pamoja na mambo mengine amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Afua za kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na wanawake kwa kipindi cha kuanzia Mwenzi Januari hadi Machi 2022.

Akaongeza kwa kusema kuwa Dawati la Jinsia la Polisi lipo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa hivyo anawaomba wananchi kutoa taarifa za Ukatili kwenye Dawati hilo popote ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwenye Vituo vya Polisi.

Kwa upande wake Mjumbe wa kikao hicho Sheikh wa Wilaya ya Ludewa Haruna Rahim amemuomba Kaimu Mwenyekiti wa kikao cha robo tatu ya kamati ya Wilaya ya Kupinga Ukatili dhidi ya Watoto na Mwanamke Ndg.Gilbert Ngailo,kuwa anaomba lianzishwe na Jukwaa la ukatili dhidi ya wanaume wanao fanyiwa ukatili lianzishwe.

Aidha wakati wa majadiliano hayo juu ya ombi la Sheikh Haruna Rahim kuomba kuanzishwe Jukwaa la Ukatili dhidi ya wanaume wanao fanyiwa ukatili lianzishwe, Mjumbe wa Kikao hicho Afisa Mradi wa Mwanamke imara kutoka Shirika la WILDAF Mkoa wa Njombe amejibu ombi la Sheikh Haruna Rahim kuwa Dawati la Jinsia na Watoto ,lipo kwa lengo la kusikiliza na kuchukua hatua stahiki kwa wale walio fanyiwa ukatili,lakini uwepo wa Dawati hilo haimaanishi kwamba wanao takiwa kwenda kupeleka ukatili huo ni watoto na wakinamama tu,Hapana bali Dawati hilo lipo kwaajili ya wote,Ukatili dhidi ya watoto,Wanawake na Wanaume.

Sambamba na hayo Mwenyekiti wa kikao hicho Ndg. Gilbert Ngailo amewasisitiza wajumbe wote kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waondokane na Ukatili kwa watu wote.

Sambamba na hayo akaongeza kwa kusema kuwa tunapo zungumzia ukatili tunazungumzia Ukatili wa Kimwili,Ukatili wa Kiuchumi,Ukatili wa Kihisia na Ukatili wa Kingono.

March 19, 2022

LUDEWA NI WILAYA ILIYO BARIKIWA NCHINI TANZANIA



Ninapo zungumzia Fursa za Uwekezaji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ninamaanisha zipo fursa nyingi kama ifuatavyo:-

Tuko na Fursa za Kilimo
Fura ya Mifugo
Fursa za Utalii
Fursa za Madini

Wilaya yetu ya Ludewa imejaliwa kuzungukwa na ukijani mbichi kila mahali na Milima mizuri inayo vutia kuitizama na kuona kama uko Dunia ya zaidi ya Dunia.

Hapa nakuangazia tu Moja ya Vivutio vinavyo tamanisha wengi kuja kutalii na mimi pia nakukaribisha sana kuja kufanya Utalii wewe mwenyewe.

Tuko na Utalii wa Ziwanyasa,Mungu hakuacha kutupatia Ziwanyasa ukanda wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ambako sasa ni Tarafa ya mwambo,huko kuna utalii ndani ya Ziwanyasa,utakutana na maji ya aina yake ndani ya ziwanyasa,Mchanga unao patikana ziwanyasa ukanda wa Ludewa ni tofauti kabisa,Utagundua Mikondo ya maji ya ziwanyasa ni tofauti na mikondo mingine iliyo zoeleka,na kwa upande wa mawe mapambo ya ziwanyasa ndio usiseme kabisa,ukiwa kama unaelekea Mbeya kule kunako itwa Makonde hauto juta kufika kutizama milima iliyo jipanga kwa ngazi moja na nyingine.

hapo nimekusogezea vichache tu ukiondoa samaki wenye rangi alimaarufu kwa samaki wa mapambo,je Utafikaje kote huko ? jibu ni kwamba Karibu Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri utapata maelekezo yaliyo jitosheleza nami nitaambatana nawe hadi kote ukutakako

Ludewa ni Wilaya iliyo barikiwa nchini Tanzania

HALMASHAURI LUDEWA YATOA VYANDUA 80 KATIKA SHULE YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM MUNDINDI



Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imetoa Vyandarua 80 katika shule ya msingi Mundindi ya watu wenye mahitaji maalum

Akikabidhi vyandurua hivyo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Gilbert Ngailo ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg Sunday Deogratias kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya shirika la PADECO.

Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Leo Machi 18, 2022 nimekuja kupokea bweni moja na pikipiki mliyo tuwezesha ninyi shirika la Padeco,tunawashukuru sana na Mkurugenzi amesema nizilete kwenu shukrani hizi,nasi kama halmashauri kwa kutambua uwepo wa watoto hawa nasi tunatoa Vyandarua hivi 80 ili kuendelea kupambana na Maralia.alisema Gilbert Ngailo.

MWENYEKITI WA CCM LUDEWA ATOA TAMKO



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ludewa Ndg. Stanley Kolimba Jana Machi 18, 2022 alizungumza na wananchi walio jitokeza katika hafla ya Miaka 10 ya shirika la PADECO walio jitokeza katika Kata ya Mundindi  shule ya msingi ya watu wenye mahitaji maalum.

Ndg.Stanlye Kolimba alisema kuwa katika kipindi cha Mwaka mmoja wa uongozi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa amefanya mambo mengi ikiwemo Miradi ya Maendeleo ya Afya,Miradi ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa na Miundombinu ya Barabara.
 
Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo aliongeza kwa kusema kuwa, tunakila sababu ya kumshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maendeleo anayo yaleta nchi kwetu haswa kwenye miradi inayo ishi, ikumbukwe kwamba Mwaka huu 2022 Mhe.Rais ametupati Fedha nyingi ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA pale Shaurimoyo ambapo ujenzi wake tayali umeanza na utarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Katika hatua nyingine Kolimba alisema Shirika la Padeco ni moja ya mashirika yanayo hitaji kuigwa haswa kwa kurudisha fadhira ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na akatumia nafasi hiyo Kumpongeza Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Wilbaard Mwinuka kwa kuendelea kuijenga Wilaya ya Ludewa kwa miradi ya kimaendeleo.

Nakupongeza kijana wetu kwa kuona umuhimu wa kuja kusaidia wototo hawa na kuwapa zawadi Bweni hili pamoja na vitanda,Magodoro 50 bado ukajenga na vyoo vitano na ukaongeza Usafiri wa pikipiki wa kuwahudimia pindi wanapo pata shida Hongera sana kijana,Sisi kama chama cha mapinduzi Wilaya ya Ludewa tunautambua Mchango wako kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa,endelea hivyo hivyo na moyo wa upendo.

Wilaya yetu inafunguka kwa mambo mengi endelea kukaribisha wageni kutoka maeneo yote waje wawekeze kwenye Halmashauri yetu uchumi Utaongezeka.


Kwa upande wake Kaimu Katibu wa wazazi CCM Wilaya ya Ludewa Ndg. Salum Mohamed Mfaume alisema kuwa uwepo wa bweni hilo ambalo Shirika la PADECO limeiwezesha shule hiyo itawafanya watoto wanao soma hapo kuishi vizuri na furaha wakiyafurahia mazingira hayo, aliendelea kusema kusema kuwa watoto ni Taifa la kesho hivyo kila mtoto aliye zaliwa anahaki ya kupata elimu kwa kauli mbiu isemayo, Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.


Bw. LINUS MALAMBA ASIMAMIA SEMINA YA UGONJWA WA POLIO


Leo Machi 19, 2022 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ludewa atoa semina ya Mafunzo kwa Kamati ya Msingi ya Afya ngazi ya Jamii (PHC) na Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ludewa akiliwakilishwa na Kaimu Das Wilaya ya Ludewa Bw. Linus Malamba



Pamoja na mambo mengine Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bw.Stanley Mlay amewaelekeza wajumbe wote walio hudhulia kikao chicho kuwa wakawe mstari wa mbele Kuongeza uelewa kwa wanajamii kuhusu faida za chanjo ya Polio.

#endelea kutembelea mitandao yetu ya kijamii kwa habari zote.

FURSA ZA KILIMO CHA KAHAWA LUDEWA

Wakati ukijiuliza wapi zinapatika fursa za kilimo hapa nchini Tanzania leo nakunong'oneza kwa ukaribu kuwa Halmashari ya Wilaya ya Ludew...